Zelensky aapa kuikwamua kusini, NATO yaonya kuhusu vita virefu

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameapa leo Jumapili kuwa vikosi vyake havitomuachia yeyote eneo lake la kusini baada ya ziara yake ya kwanza katika maeneo hayo. Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ameonya kuwa vita vya Urusi nchini Ukraine vinaweza kudumu kwa miaka mingi. Jeshi la Ukraine limesema Urusi imezidisha mashambulizi yake katika mji wa viwanda wa Severodonetsk, lengo kuu likiwa ni kuudhibiti kikamilifu mkoa wa Luhansk, mmoja wa mikoa miwili inayounda ukanda wa Donbas. Gavana wa Luhansk Serhiy Gaidai amesema hali ya Severodonetsk ni ngumu sana.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii