Wanajeshi wa Sri Lanka wafyatua risasi kudhibiti ghasia za mafuta

Wanajeshi wa Sri Lanka walifyatua risasi katika mji wa Visuvamadu, karibu kilometa 365 kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Colombo ili kudhibiti ghasia katika kituo cha mafuta ambako kulishuhudiwa foleni kubwa za kununua mafuta ya petroli na dizeli. Polisi wamesema kuwa raia wanne na wanajeshi watatu walijeruhiwa. Sri Lanka inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi tangu ilipojipatia uhuru wake, na ina uhaba wa fedha za kigeni ili kuagiza bidhaa muhimu kama chakula, mafuta na madawa. Kwa miezi kadhaa Rais wa nchi hiyo Gotabaya Rajapaksa amekuwa akipinga wito wa kujiuzulu kutokana na usimamizi mbovu huku serikali yake ikiwaweka polisi wenye silaha na wanajeshi kulinda vituo vya mafuta.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii