Kansela Scholz atetea msimamo wa Ujerumani juu ya kupeleka silaha Ukraine

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametetea mchango wa nchi yake katika kuipelekea silaha Ukraine na ameahidi kupeleka silaha zaidi pamoja na mfumo wa kisasa wa ulinzi wa anga. Katika hotuba aliyotoa bungeni, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia alifafanua sera ya nchi yake juu ya vita vya nchini Ukraine, athari za kiuchumi zilizosababishwa na vita hivyo na mpango wa serikali yake juu ya matumizi kwa ajili ya wananchi. Ujerumani imekuwa inalaumiwa kwa kusuasua kuipelekea Ukraine silaha nzito lakini Kansela Scholz amesema Ujerumani imekuwa inapeleka silaha Ukraine muda mfupi baada ya vita kuanza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii