Hali ya wasiwasi kati ya Wapalestina na Waisraeli yaripotiwa Mashariki mwa Jerusalem

Maelfu ya Waisraeli, wakiwa wanapeperusha bendera ya nchi yao, wameandama katika eneo la Wapalestina, Mashariki mwa Jerusalem, katika kitendo ambacho kimelezwa kuwa cha kichokozi. 


Maandamano hayo yamelaaniwa na uongozi wa Mamlaka ya Palestina, ambao umesema Israeli, inacheza na moto, huku kukiwa na makabiliano kati ya Waisraeli na Wapalestina. 

Waisraeli wakiwa na bendera ya nchi yao, huadamana Mashariki mwa Jerusalem, kila tarehe 29 Mei, kukumbuka namna walivyoteka eneo la Mashariki mwa Jerusalem wakati wa vita vya 1967.

Israeli imeendelea kusisitiza kuwa eneo lote la Jerusalem, ni mji wake mkuu, licha ya kupingwa na baadhi ya nchi, ikiwemo Palestina.

Hii imekuja wakati huu kukiendelea kushuhudiwa kwa hali ya wasiwasi kati ya Wapalestina na Waisraeli, kufuatia mapigano ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakishuhudiwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii