Siku ya 96 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu Mei 30, Ukraine imedai kurejesha kwenye himaya yake eneo la Kherson, kutoka mikononi mwa Urusi tangu kuanza kwa uvamizi huo.
Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna, atazuru mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na Bucha siku ya Jumatatu. Atakutana na Rais Volodymyr Zelensky.
Ukraine imedai kurejesha kwenye himaya yake eneo la Kherson, kutoka mikononi mwa Urusi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi, karibu na vijiji vya Andriyivka, Lozove na Bilohirka. Mashambulizi haya yanakuja wakati mamlaka mpya ya jiji, iliyoteuliwa na Kremlin, tayari imeelezea nia ya kuunganishwa na Urusi.
Siku moja baada ya ziara yake huko Kharkiv, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzungumza mwanzoni mwa mkutano wa kilele wa Ulaya siku ya Jumatatu, kwa njia ya video kutoka mjini Kyiv. Vikwazo vipya dhidi ya Moscow viko kwenye ajenda ya mkutano huu wa nchi Ishirini na Saba.
Vikosi vya Urusi vinasonga mbele kuelekea katikati mwa mji wa Sievierodonetsk, gavana wa eneo hilo alimesema leo Jumatatu. Mji huu katika mkoa wa Luhansk umekumbwa na makombora kwa siku kadhaa, baada ya kutekwa kwa eneo muhimu la Lyman, hali ambayo inafungua njia kuelekea miji mikubwa ya Sloviansk na Kramatorsk.