Mbunge wa Rabai Aaga Dunia Baada ya Kuwasilisha Stakabadhi kwa IEBC.

Mbunge wa Rabai William Kamoti amefariki dunia muda mfupi baada ya kuwasilisha karatasi zake za uteuzi kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka.
OCPD wa Kilifi Jonathan Koech alithibitisha kifo cha mbunge huyo kilichosababishwa na ajali mbaya ya barabarani katika eneo la Mnarani kando ya barabara kuu ya Maziwa-Mombasa-Malindi jioni ya Jumapili, Mei 29
Seneta James Orengo alisema: "Rambirambi zangu za dhati kwa familia, marafiki na wananchi wa eneo bunge la Rabai kufuatia kifo cha mbunge wao Mhe.William Kamoti Mwamkale. Tumempoteza mtumishi wa wananchi mwenye bidii na shauku. Roho yake ipumzike kwa amani. "
Mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM Philip Etale alisema: "RIP rafiki yangu Mheshimiwa. William Kamoti, Mbunge wa Eneo Bunge la Rabai katika kaunti ya Kilifi. Bwana mwema ametuacha. Huzuni. Pole kwa wakazi wa Rabai."

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii