Ndege yenye watu 22 imepoteza uelekeo nchini Nepal. Kwa mujibu wa shirika la ndege la taifa hilo ndege hiyo ilipoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kuruka saa tatu na dakika 55 ya leo katika uwanja wa ndege wa mji wa magharibi wa Pokhara ikielekea katika eneo la kitalii la Jomsom. Msemaji wa shirika hilo lijulikano kwa ufupi Tara Air, Sudarshan Bartaula amesema ndege hiyo inayofanya safari za ndani ilikuwa na abiria 19 na wahudumu watatu. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Phanindra Mani Pokharel, amesema helkopta mbili zimepelekwa katika eneo la tukio lakini matumani ya kupatikana kwa ndege hiyo ni madogo.Amesema hali mbaya ya hewa inatatiza shughuli za utafutaji. Jomson ni sehemu maarufu ya katika milima ya Himalaya, ambayo ipo umbali wa dakika 20 kwa ndege kutoka Pokhara, kwa upande wa magharibi ya Kathmandu.