Watu 19 wamefariki dunia baada ya basi dogo aina ya Costa kugongana kugonga lori lililokuwa limeharibika karibu na eneo la Changarawe, Mafinga mkiani Iringa.
Akizungumza i leo Ijumaa Juni 10, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amethibitisha kutokea vifo hivyo akisema kuwa taarifa ziaidi zitatolewa baadaye
"Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo," amesema.
a watu walio katika eneo la tukio wamesema mpaka saa tatu asubuhi, jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mafinga Dk, Victor Msafiri amethibitisha kupokea miili hiyo pamoja na majeruhi nane katika hospitali hiyo.
Dk Masafiri amesema majeruhi wawili wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa ajili ya matibabu zaidi.