Katika siku ya 106 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Alhamisi Juni 9, fuata moja kwa moja taarifa za hivi punde kuhusu mzozo huo.
Wanajeshi wa Ukraine wanapigana huko Sievierodonetsk moja ya "vita ngumu zaidi" tangu kuzuka kwa vita kupinga vikosi vya Urusi ambavyo sasa vinadhibiti sehemu kubwa ya mji huu wa kimkakati wa mashariki ambapo, kulingana na Rais Volodymyr Zelensky, "hatma" ya eneo la Donbass iko hatarini.
Urusi imesema iko "tayari" kuhakikisha usalama wa meli za nafaka zinazoondoka kwenye bandari za Ukraine, kwa ushirikiano wa Uturuki, alisema Waziri wake wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov siku ya Jumatano, wakati alikuwa akikutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Uturuki mjini Ankara. Lakini mkutano huo haukuwezesha kuanzishwa kwa maeneo salama ya kibinadamu baharini yatakayowezesha usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi.
Zaidi ya wanajeshi 1,000 wa Ukraine, ambao walikuwa wamekamatwa huko Mariupol, wamehamishiwa Urusi ambako watakuwa chini ya uchunguzi, kulingana na shirika la habari la Urusi la TASS.
Uchumi wa dunia unazidi kudorora zaidi kutokana na vita vya Ukraine na kuna hatari ya kuagusha kabisha kwa uchumi huo, linaonya shirika la OECD katika utabiri wake wa hivi karibuni, ucghumi ambao unatarajia kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa kimataifa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei Mwaka huu.