mwanamke wa India amtusi Mtume Muhammad

India inakabiliwa na shinikizo la kidiplomasia kuhusu matamshi yenye utata yaliyotolewa na afisa w angazi ya juu wa chama tawala cha nchi hiyo - Bharatiya Janata Party (BJP) ambaye alimtusi Mtume Mohammad.

Nupur Sharma alizitoa kauli hizo siku 10 zilizopita baada ya kushiriki katika mdahalo wa televisheni, ambayo yamewakera Waislamu nchini India, na zaidi ya makumi kadhaa yan chi za Kiislamu.

Jumapili chama cha BJP kilimsimamisha kazi Bi Sharma. Mkuu wa habari wa chama tawala nchini , Naveen Kumar Jindal, pia a,esimamishewa kazi kwa kutuma picha za matusi.

BJP kilisema katiika taarifa yake kuwa "kinapinga mawazo yoyote yanayotusi au kudharau kikundi au dini ," na kuongeza kuwa "hakiwaungi mkono watu hao au farsafa wanazoziamini."

Wanadiplomasia wa India wanajaribu kuzishawishi nchi za Kiislamu ambazo zimekasirishwa na kosa la kudhihakiwa kwa Mtume kutambua kuwa matamshi hayo hayaonyeshi msimamo wa serikali ya na kwamba hayo ni "maoni ya itikadi kali"

Kabla ya kufutwa kazi, Nupur Sharma ambaye ni mwanasheria mwenye umri wa miaka 37, alikuwa ni mtu mashuhuri "msemaji wa BJP " ambaye amekuwa akionekana mara kwa mara hasa nyakati za usiku kwenye vipindi vya televisheni kuitetea serikali ya Waziri mkuu wa India Nahendra Modi

Alipokuwa akisoma katika chou kikuu cha Delhi, Sharma alianza safari yake ya kisiasa katika mwaka 2008 wakati alipochaguliwa kuwa rais wa wanafunzi wa chama cha Akhil Bharatiya Vidyarthi Parishad (ABVP), ambalo ni vuguvugu la Wahindu la Rashtriya Swayamsevak Sangh.

Mwaka 2011 alisoma shahada ya uzamifu nchini India, ambapo alitumukiwa shahada ya uzamifufu ya sheria ya kimataifa ya kimataifa kutoka Chuo cha masuala ya Kiuchumi cha London- London School of Economics.

Mnamo mwaka 2013 alikuw amjumbe wa kamati ya habari ya chama tawala cha PJP, na hapo aliweza kushiriki katika mdahalo wa televisheni unaofanyika katika lugha za Kihindu na Kiingereza.

Miaka miwili baada ya kutangazwa upya kwa uchaguzi, alikuwa mgombea wa BJP dhidi ya kiongozi wa Delhi Arvind Kejriwal.

Haukuwa ucgaguzi ambao yteyote alitarajiw akushinda, lakini kampeni yake imara ilimfanya ateuliwe kuwa Msemaji rasmi wa chama mjini Delhi, na mwkaa 2020 akawa "Msemaji wa taifa" wa BJP.

Ghadhab ya Ulimwengu wa Kiislamu

Kuwait, Qatar na Iran oJumapili ziliwaita mabalozi wa India kuelezea hasira zao. Saudia pia ililaani kauli zilizotolewa na Sharma, na Qatar inasema inategemea Idia iombe radhi kwa umma.

"Kuruhusu chuki dhidi ya Uislamu kuenedelea bila kukomeshwa, inatishia haki za binadamu, na inaweza kupelekea chuki zaidi na ubaguzi, jambo linalosababisjha ghasia na chuki zaid", ilisema wizara ya mambo ya nje ya Qatar.

Saudi Arabia pia imeelezea kukasirishwa kwake na kitendo cha Sharma. "Wizara ya mambo ya nje inalaani vikali matamshi yaliyotolewa na msemaji wa chama cha cha Bharatiya Janata (BJP) nchini India, kumtukana Mtume Mohammad, rehema na amani viwe juu yake, na tunaendelea kukataa chuki dhidi ya Uislamu." ilisema.

Balozi wa India nchini Qatar, Deepak Mittal, amesema kuwa matamshi yaliyotolewa na baadhi ya 'wenye chuki' hayaoneshi maoni ya serikali ya India. Viongozi wa ngazi ya juu wa BJP na mabalozi wengine pia walilaani kauli tata zilizotolewa na Bi Sharma.

Lakini wachambuzi wanasema uongozi wa juu wa chama na serikali huenda wakalazimika kuongea wazi . "kama hili halitafanyika," wanasema, " inaweza kuharibu vibaya mahusiano ya kidiplomasia kati ya India na mataifa haya''

Wakati huo huo na Rais wa Urusi Vladimir Putin pia alielezea a kutofurahishwa kwake na matamshi yenye utata kumuhusu Mtume Mohammad katika serikali ya India.

Bw Putin aliishauri India wakati wa mkutano wake wa mwaka na waandishi wa habari, alisema, "Matusi dhidi ya Mtume Mohammad ni ukiukaji wa uhuru wa dini na kuwakashifu Waislamu. "

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii