Mwanamume mmoja alizirai na kuaga dunia akifanya mazoezi katika ukumbi wa mazoezi maarufu kama gym kwenye barabara ya Koinange jijini Nairobi.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 51 na kukimbizwa kwa hospitali moja iliyokuwa karibu lakini akaripotiwa kuwa amefariki tayari.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, mwendazake amekuwa akifanya mazoezi katika ukumbi huo kwa muda na alizirai alipokuwa akifanya mazoezi kwenye mashine ya kukimbia.
Polisi wanasema kuwa wanapanga kuufanyia mwili huo upasuaji ili kubaini kiini cha kifo hicho