Jeshi la Korea Kusini limesema leo kuwa Korea Kaskazini imefyetua kombora la masafa marefu kwenye bahari Mashariki mwa Pwani yake hili likiwa tukio la hivi karibuni zaidi katika mfululizo wa majaribio ya silaha. Korea Kaskazini imepunguza maradufu mpango wake wa uboreshaji silaha mwaka huu licha ya kukabiliwa na vikwazo vya kiuchumi. Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wameonya kwa wiki kadhaa kwamba huenda Korea Kaskazini ikafanya jaribio la saba la nyuklia. Mwezi uliopita, Korea Kaskazini ilifanyia majaribio makombora matatu na uwezekano wa kombora lake kubwa zaidi la, Hwasong-17.Majaribio hayo yamefanyika siku chache baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuondoka Korea Kusini kufuatia mkutano na Rais mpya mteule Yoon Seok-you