MWANAFUNZI AINGIA NA BOMU LA MACHOZI DARASANI

Polisi eneo la Changamwe katika Kaunti ya Mombasa wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne aliingia shuleni na kitoa machozi.
Kwa mujibu wa Naibu Kaunti Kamishna wa Changamwe Michael Yator, mwanafunzi huyo wa Shule ya Upili ya St. Charles Lwanga aliingia shuleni humo na kitungi cha kitoa machozi mnamo Ijumaa asubuhi.
Mwanafunzi huyo alienda kucheza na kitungi hicho akiwa na wenzake, kikilipuka na kujeruhi wanafunzi watano akiwemo yule aliyekuwa ameingia nacho shuleni kisiri.
Yator anasema kuwa wanafunzi hao walipata majeraha madogo madogo na kwa sasa wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Bomu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii