Hospitali ya Kitaifa ya Abuja, siku ya Jumatatu, Mei 16, ilikanusha madai kuwa maiti ya mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, Osinachi Nwachukwu, ilikuwa ikiimba ‘Ekwueme’ katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Msemaji wa hospitali hiyo, Dkt Taiwo Haastrup, alisema hakuna uthibitisho kwamba mwili wa Osinachi ulikuwa ukiimba katika chumba cha kuhifadhi maiti, The Punch inaripoti.
Akiongea na wanahabari, Haastrup alibainisha kuwa mtu aliyekufa hawezi kuimba akiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Osinachi, mwanakwaya katika Kanisa la Kimataifa la Dunamis, alifariki miezi michache iliyopita kutokana na kile kinasemekana kuwa unyanyasaji wa nyumbani aliofanyiwa na mumewe, Peter Nwachukwu.
Kufuatia kifo chake, mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Taifa.
Ripoti zilienea kwamba wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti walidai kuwa maiti ya Osinachi iilikuwa ikiimba wimbo wake wa 'Ekwueme', usiku wa manane.
Akijibu ripoti hiyo, Haastrup alisema: “Kitiba, hakuna kitu kama hicho; ni mawazo ya watu tu. Mtu ambaye amekufa na ni maiti, mtu kama huyo atakuwa anaimbaje usiku?"
"Hakuna chelezo ya matibabu kwa hilo; ni mawazo ambayo yanaweza kuwa ni kutokana na kanisa alilohudhuria akiwa hai, na nyimbo zinaweza tu kuwapa watu mawazo, lakini hakuna uthibitisho kwa njia yoyote. Haiwezi tu kuthibitishwa kwa njia yoyote. “Mtu aliyekufa amekufa na amekuwa maiti; iko ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, haiwezi kuimba na haiwezi kusonga kwa hivyo ni mawazo ya watu."
Kuhusu ripoti ya uchunguzi wa maiti, Hasstrup alisema:
"Ni kesi ya uchunguzi, na ni siri; hatuwezi kufichua chochote hapo. IPO anayehusika atampa IGP, ambaye atapeleka mahakamani. Matokeo yamewasilishwa sawa, na watu wetu walifanya hivyo kwa siri."