Nchini Burkina Faso, ukatili dhidi ya raia umeongezeka kwa kasi katika muda wa miezi tisa iliyopita, kulingana na uchunguzi wa hivi punde wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch, uliochapishwa Jumatatu, Mei 16, 2022.
•HRW iliwahoji watu 83 walionusurika katika matukio ya usalama yaliyotokea kati ya mwezi Septemba 2021 na mwezi Aprili 2022, katika mikoa sita ya nchi. Wataalamu wa afya, wachambuzi wa usalama, maafisa wa serikali, wanadiplomasia wa kigeni, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada pia walihojiwa.
Inaonekana kutokana na utafiti huu kwamba raia wanazidi kulengwa, sio tu na makundi ya kigaidi, bali pia na vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na watu wa kujitolea kwa ulinzi wa taifa.
Makundi ya Kiislamu yenye silaha yamejaribu kuchukua udhibiti kutoka kaskazini hadi katikati mwa nchi. Wanashambulia vijiji vidogo na pia jiji kubwa zaidi, kwa mfano Dablo, Namissiguima. Kwa hiyo walitangaza sheria yao kwa watu kuondoka, na kwa kuwa hawakuondoka, walivamia kijiji. Pia kuliripotiwa visa vya watu 42 waliouawa na 14 waliotoweka kitendo kilichofanywa na vikosi vya usalama, akiwemo waziri anayeunga mkono serikali. Matukio mengi yalichochewa katika operesheni za kukabiliana na ugaidi. Wengi wa waathiriwa walikuwa wakilengwa kwa madai ya kuajiriwa katika kundi la wanajihadi. Kuanzia mwaka 2020, mauaji yanayotekelezwa na vikosi vya usalama yamepungua sana. Lakini yalianza kuongezeka tena mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana, amesema Corinne Dufka, mkurugenzi wa Human Rights Watch katika ukanda wa Sahel.