Ukraine yaongeza juhudi za uokozi Azovstal

Juhudi zinaendelea kuwaokoa wapiganaji wa mwisho wa Ukraine ndani ya kiwanda cha chuma cha pua cha Azovstal katika mji ulioharibiwa na vita wa Mariupol. Hii ni baada ya maafisa wa Ukraine kusema wapiganaji hao walikuwa wamekamilisha kazi na hakukuwa na njia nyingine ya kukikomboa kiwanda hicho kutumia mbinu za kijeshi. Jeshi la Ukraine limejiepusha kutumia neno kujisalimisha kuelezea juhudi za kuondoka Azovstal kwa nia ya kuyaokoa maisha ya watu wengi kadri inavyowezekana. Haijafahamika ikiwa wanajeshi waliopelekwa katika maeneo yanayodhbitiwa na Urusi watachukuliwa kama wafungwa wa kivita. Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine alisema jana kwamba zaidi ya wapiganaji 260, baadhi yao wakiwa na majeraha mabaya, waliondolewa kutoka kiwandani hapo na kupelekwa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Urusi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii