Raia wa Tunisia wameandamana katika jiji la taifa hilo Tunis, kupinga hatua ya rais Kais Saied kuendelea kujilimbikizia madaraka na kupanda kwa gharama ya maisha.
Vuguvugu linaloongoza maandamano hayo la Ennahda kupitia kwa mmoja wa maafisa wake Ali al Arid, limesema maandamano hayo yataendelea yakihusisha kususia chakula hadi pale rais Saied atakaporejesha mfumo wa demokrasia.
Raia walioshiriki maandamanao hayo ya jana wameonekana wameshika bendera ya taifa hilo na mikate kama ishara ya kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.
Rais Saied amekuwa akifanya mabadiliko nchini Tunisia, baada ya kulivunaja bunge, baadhi ya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuvunja baadhi ya taasisi za serikali.
Mapema mwezi huu rais Saied alitangaza mpango wa kuundwa kwa Tunisia mpya, kupitia kura ya maoni itakayofanyika Julai 25.