Mwanasiasa Wa Kenya Awatepeli Mawakala wa M-Pesa Zaidi ya KSh 350k Read.

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wamemkamata mwanasiasa mmoja kwa kujipatia zaidi ya KSh350,000 kwa njia ya ulaghai kutoka kwa maajenti wa Mpesa.
Benson Thuranira Kathiai anadaiwa kuwatepeli maajenti wa Mpesa katika terehe mbalimbali.
Kulingana na maafisa hao Thuranira, mwanachama wa chama cha Narc Kenya atakuwa chini ya ulinzi wa polisi hadi Jumatatu, Mei 30, atakapofikishwa mahakamani.
"Benson Thuranira Kathiai, ambaye ndiye bosi wa genge la walaghai maarufu mjini Nakuru, linalojulikana kama Confirm atakuwa mgeni wetu hadi Mei, 30 atakapojibu mashtaka ya utapeli katika mahakama za Nakuru," DCI iliripoti.
Thuranira ambaye anawania kiti cha wadi ya Muthara alikamatwa na maafisa wa upelelezi.
Kukamatwa kwake kulijiri kufuatia malalamishi mengi kutoka kwa maajenti wa Mpesa waliouwa wamepoteza hela zao mikononi mwa mshukiwa huyo.
Mgombea huyo wa MCA anasemekana kujipatia KSh 100,000 kwa njia ya ulaghai mjini Nakuru kutoka kwa maajenti wawili wa Mpesa kabla ya kupata KSh 135,000 zaidi huko Shauri Moyo, KSh 60,000 Busia na KSh 120,000 Meru kabla ya kukamatwa.
Maafisa wa DCI walioko Nakuru wametoa wito kwa maajenti wengine wa Mpesa ambao Thuranira huenda aliwalaghai kujitokeza na kuwasilisha ripoti zao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii