• Ijumaa , Agosti 1 , 2025

Kanisa Laadhimisha Sikukuu ya Krismasi nchini Congo.

Kanisa moja nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo limeadhimisha Sikukuu ya Krismasi likisherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristu.
Tofauti na kawaida ambapo makanisa mengi ulimwenguni huadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristu mnamo Disemba 25 kila mwaka, waumini wa Kanisa la Church of Jesus Christ on Earth liliadhimisha sikukuu hiyo mnamo Mei 25,  Jumatano nchini Congo na Angola


Mwasisi wa kanisa hilo nabii Simon Kimbangu ana wafuasi wapatao milioni 20 nchini Congo ambayo ndio makao makuu na pia anajivunia wafuasi wengine kadhaa katika nchi jirani ya Angola
Kanisa hilo lilibandikwa jina Kimbanguist kutokana na jina la mwasisi wake nabii Simon Kimbangu ambaye mnamo Aprili 1921 alianzisha vuguvugu la watu wengi kupitia uponyaji wake wa kimiujiza na mafundisho ya kibiblia.


Waumini wa kanisa hilo hujiepusha na vita siasa na kukumbatia imani katika thamani ya maadili ya kazi, kukataa ujeuri, ndoa za mitala, uchawi, pombe, tumbaku, na densi.
Ibada yao ni ya Kibaptisti kwa kiwango fulani, japo hawakuwa wanatumia komunyo hadi mwaka wa 1971.


Kulingana na waumini wa kanisa hilo, nabii Simon Kimbangu anasemekana alishuka duniani kutoka Mlima Sayuni akiwa mtoto mchanga wa Congo
Waumini hao pia wanaamini kuwa Simon Kimbangu ni Roho Mtakatifu, aliyetajwa kwa mujibu wa Yohana 14:15-17.


Sawia vikundi vingi vya Kikristo, Wakimbangu huanza na kumaliza maombi yao wakitaja jina la Baba la Mwana na Roho Mtakatifu.
Hali ya kimafundisho iliyotolewa na kanisa hili kwa Simon Kimbangu imesababisha mabishano ya kimataifa kinyume na fundisho la Utatu na kwa hiyo kuzua uzushi.


Mnamo 2021, uanacham wa kanisa hilo katika Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) ulifutwa na halmashauri kuu ya WCC kwa misingi ya kitheolojia.
Tarehe tatu muhimu katika kalenda ya kanisa hilo ni Aprili 6 ambayo huashiria tarehe ya kuanza kwa huduma ya uponyaji), 25 Mei kuashiria Krismasi ambayo ni siku ya kuzaliwa kwa Padre Dialungana), na 12 Oktoba ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kimbangu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii