AJALI mbaya imetokea inayohusisha gari aina ya TOYOTA PICKUP lenye namba ya usajili T 840 DQF lililokuwa likitokea maeneo ya Tumbaku kuelekea Msamvu kugonga Behewa la Treni lililokuwa likitokea Kilosa kuelekea Stesheni ya Morogoro.
Tayari Askari wa Usalama Barabarani wameshafika eneo la tukio na shughuli za uokoaji zimeendelea sambamba na uchunguzi wa tukio hilo.