Jeshi la Mali limezuia vikosi vya UN kufanya doria kwenye kiini cha ghasia za wanajihadi

Jeshi la Mali lilizuia vikosi vya Umoja wa Mataifa kufanya doria katika mji wa kati wa Djenne kiini cha ghasia na harakati za wanajihadi katika Sahel msemaji wa UN alisema Alhamis tukio la karibuni katika mifululizo ya shughuli zake huko.

Tukio hilo linakuja wiki chache kabla ya mjadala wa UN kuhusu iwapo itarejesha mamlaka ya ujumbe wake nchini Mali huko vikwazo vilivyowekwa dhidi yake na serikali ya kijeshi vinatarajiwa kuchangia katika uamuzi huo.

Afisa wa jeshi la Mali katika eneo hilo alisema doria hiyo iliahirishwa tu akilaumu kucheleweshwa kwa shughuli za kijeshi na kwa tume ya MINUSMA.

Wanajeshi wa Mali katika miezi ya karibuni wameigeukia Russia na kukaa mbali na Ufaransa kwa ajili ya kuungwa mkono katika mapambano yake dhidi ya jihadi.

Afisa wa usalama akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kwamba MINUSMA haikuwahi kushuhudia matatizo katika doria ya Djenne.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii