Utafiti mpya umegundua kuwa uchafuzi wa mazingira wa aina zote ndio chanzo cha vifo vipatavyo milioni 9 kwa mwaka duniani kote. Idadi hiyo ya vifo imehusishwa na sababu za hewa chafu kutoka kwenye magari na ambayo imepanda kwa asilimia 55 tangu mwaka 2000. China inaongoza duniani kwa vifo vya uchafuzi wa mazingira. Marekani ni ya saba kati ya nchi 10 zilizoendelea kiviwanda katika kusababisha vifo vinavyotokana na uchafuzi wa mazingira. Bangladesh na Ethiopia pia zimetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazosababisha vifo kwenye utafiti huo mpya ulioorodheshwa katika jarida la Lancet. Nchi nyinginezo zilizotajwa kwenye utafiti huo ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, Brunei, Qatar na Iceland zikiwa na kiwango cha chini zaidi cha vifo vinavyosabaishwa uchafuzi wa mazingira.