Mamlaka yenye kushughulika na majanga nchini Afghanistan imesema mvua kubwa na mafuriko yamesababisha vifo vya watu watu 22, kuharibu mamia ya nyumba na mazao, katika taifa hilo ambalo tayari limekuwa likikabiliwa na janga la kiutu.Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika mamlaka hiyo, Hassibullah Shekhani, amesema mafuriko na dhoruba vimeyakumba majimbo 12, ambapo pamoja na idadi hiyo ya vifo watu wengine 40 wamejeruhiwa.Maafisa wanasema serikali ya Taliban ambayo ipo katika kukabliana na athari ambazo zinayakabili zaidi ya theluthi moja ya majimbo yake, itapaswa kuwasiliana na mashirika ya kimataifa kwa kuomba msaada.Kwa kawaida mvua na mafuriko vinakuwa vya kiwango cha juu sana katika maeneo ya magharibi majimbo ya Badghis na Faryab na jimbo la kaskazini la Baghlan.