Mkulima Ukraine Aibiwa Trekta na Majeshi ya Urusi Linaloendeshwa kwa Rimoti

Majeshi ya Urusi katika mji unaoshikiliwa na majeshi hayo wa Melitopol yamegundulika kuiba Trekta la mkulima mmoja nchini Ukraine lenye thamani ya Dola milioni 5 wakiwa na lengo la kulipeleka Chechnya.

Taarifa zinadai baadaye iligundulika baada ya safari ya maili 700 wezi hao walishindwa kabisa kutumia vifaa hivyo vya Trekta kutokana na kufungwa na rimoti.

Kwa kipindi cha wiki kadhaa kumekuwa na taarifa ya majeshi ya Urusi kuiba zana za shambani, mazao lakini pia vifaa vya ujenzi kwa raia wa Ukraine, lakini kuibiwa kwa zana hizo za kilimo katika shamba la John Deere mjini Melitopol kumefanikishwa na magari ya kijeshi ya Urusi.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Marekani CNN linadai kuwa zana hizo ziliibiwa na majeshi ya Urusi mapema mwezi Machi kutoka Kampuni ya Uuzaji wa zana za shamba ya Agrotek iliyopo mjini Mariupol.

CNN imeshindwa kuweka wazi jina la shuhuda wa tukio hilo la wizi lililotekelezwa na majeshi ya Urusi kwa ajili ya kulinda usalama wake,

Shuhuda huyo alisema:

“Zana zilizosafirishwa kwenda Chechnya ambazo zinahusisha mashine ya kuvuna na kupakia inaendeshwa kwa rimoti lakini inasemekana kuwa wameshatafuta mtu wa kuwasaidia kutatua tatizo hilo, hata kama wakiamua kuuza kama mabaki bado watapata pesa nyingi tu.”

Shuhuda mwingine ameiambia CCN kuwa wezi hao kutoka majeshi ya Urusi wamekuwa wakiwalaghai wakulima na kuwaibia mazao yao kwani kwa wakulima ambao wanaendelea kufanya shughuli za uzalishaji katika miji ambayo ipo chini ya Utawala wa majeshi ya Urusi hawawezi kufanya chochote na mazao yao.

Ameendelea kueleza kuwa hakuna kitu chochote kinachofanyika ndani ya miji hiyo hata Bandari nayo haifanyi kazi kiasi kwamba mazao hayawezi kutoka ndani ya miji hiyo.

Mjeshi ya Urusi yanalaumiwa na Jumuiya za Mataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa UN kutokana na kutekeleza matendo ya kikatili dhidi ya raia wa Ukraine japo kwa muda mrefu Urusi imekuwa ikikanusha madai hayo ya kuwadhuru raia ikidai inaendesha operesheni maalum dhidi ya raia wa Ukraine wenye mlengo wa kinazi ambao unahatarisha usalama wa Urusi.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii