Mwizi wa Viatu Msikitini Apewa Adhabu ya Kula Pilipili Mwaka.

Baadhi ya wakaaji wa Mombasa sasa wameanza kuitumia pilipili kama kifaa cha kuadhibu watu wanaokutwa na makosa kwa mfano wizi.
Waliomkamata katika tendo hilo walimlazimisha kukiri kuiba kabla ya kumpa pilipili hiyo kuila na kumtaka aseme hatowahi kurudia tena.
"Mimi ni mwizi na mimi huiba viatu, nilitumwa na Felix anayefanya kazi feri. Baadhi ya viatu ninavyoiba sisi huviuza feri na Changamwe," alisema mwizi huyo chini ya ulinzi mkali.
Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa adhabu ya aina hii kutumika na itakumbukwa katika kisa kingine cha wizi, jamaa alitakiwa kuchagua kati ya kupigwa kitutu na kula pilipili.
La kushangaza ni kuwa, jamaa huyo alichagua kula bakuli la pilipili huku waliokuwa wamemkamata wakiangalia.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii