Kenya yamuaga Mwai Kibaki.

Kenya leo inamuaga rasmi rais wa zamani wa nchi hiyo Mwai Kibaki aliyefariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 90. Viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika wanatarajiwa kushiriki shughuli hiyo inayofanyika katika uwanja wa michezo wa kitaifa wa Nyayo jijini Nairobi. Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Salva Kirr wa Sudan Kusini sambamba na mabalozi, maafisa na viongozi wa kiserikali. Malkia wa Uingereza Elizabeth wa Pili jana Alhamisi alituma ujumbe wake wa salamu za rambirambi kwa Rais Uhuru Kenyatta ambapo aliisifu rekodi ya Mwai Kibaki katika majukumu yake ya kuwatumikia Wakenya. Rais huyo wa zamani wa Kenya atazikwa kesho Jumamosi kwake katika mji wa Othaya, kaskazini mwa Nairobi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii