Tunajivunia pia kwa ya hivi karibuni kuongeza thamani katika
uwekezaji huo kwa kuongeza kipengele cha utoaji wa bima za afya na
maisha kwa wachezaji wa ligi hiyo. Shukrani kwa TFF na washirika wetu wa
kampuni za Bima za Sanlam na Britam kwa kuwezesha utoaji wa Bima hizo
ambazo pia zitahusisha wafanyakazi wa klabu, na familia zao.
Timu 16 zinazoshiriki katika Ligi Kuu ya
NBC, zina jukumu muhimu katika maendeleo na ustawi wa jamii zao
kiuchumi na kijamii. Biashara mbalimbali katika miji yenye timu hizi
huneemeka sana kwa uwepo wa mechi katika miji yao na hivyo kuasaidia
sana kuongeza vipato vya familia.
Ligi
hii yenye jumla ya michezo 240 iliyoenea nchini kote kuanzia Dar mpaka
Geita hadi Mpanda, imekuwa ni msaada mkubwa katika mapato na hivyo
kusaidia kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhidi ya umaskini.
Ripoti
ya hivi karibuni alionyesha kuwa moja ya mechi kubwa kabisa nchini,
miaka michache iliyopita iliyohudhiriwa na zaidi ya watu 59,000,
iliingiza mapato ya kiasi cha shilingi 545,422,000 na hivyo kuingiza
kodi kubwa kwenye kapu la Serikali.
Huu ni mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.
Pia
kuna zaidi ya ajira 3,000 za moja kwa moja kwa wachezaji, waamuzi,
wauguzi, na walimu. Ikiwa ukubwa wa wastani wa kaya nchini watu wa tano
au zaidi kwa kaya, ligi ya NBC inasimama kama chombo cha kupunguza
umaskini, kuboresha ustawi wa kaya, na kuboresha viwango vya maisha.
Mamilioni
ya ajira zingine zisizo za moja kwa moja zinaundwa katika minyororo ya
uchumi kupitia bidhaa kama chakula, mavazi, malazi, utangazaji, wachuuzi
na mengineyo.
Benki ya NBC pia
inajivunia kutumia jukwaa hili katika kuunga mkono juhudi za Serikali
kusukuma ajenda ya ujumuishaji wananchi katika sekta rasmi ya fedha.
Kupitia mechi za ligi hii, tumefanikiwa kukutana na wanachi wengi zaidi
kuliko hapo awali. Mpira wa miguu unasimama kama jukwaa muhimu sana
katika kuwafikia ambao walikuwa hawajafikiwa na elimu rasmi juu ya
masuala ya fedha na uwekezaji.
Ligi
Kuu ya NBC pia inajumuisha mchanganyiko wa nyota wa kimataifa na vipaji
vya nyumbani. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linaitaja ligi hii kwa
kuashika nafasi ya nane bora barani Afrika. Wakati huo huo, klabu za
Yanga na Simba zinaongoza kwa kuwa na amshabiki wengi zaidi zaidi
Afrika Mashariki na Kati.
Ni
wakati wa muafaka sasa kuanza kubadili umaarafu huu nchi za jirani kuwa
chanzo cha fedha za kigen na mapato kwa taifa kupitia utalii wa
michezo. Ligi Kuu ya Uingereza ilipata dola milioni 602 kutoka kwa
mashabiki wa kimataifa wanaosafiri kwenda kwenye michezo.
Uwepo
wa majina makubwa ya nyota wa kigeni wanaocheza katika ligi yetu ya
NBC, Umaarufu wa ligi yetu kimataifa, ikijumuishwa na mazingira bora ya
usafiri na amani nchini, vinaweza kuwa vivutio tosha kuleta watalii wa
michezo nchini kutazama mechi zetu kubwa na baadaye kutembelea vivutio
vyetu vya utalii.