Sababu ya Mwanri Kuamrisha Shamba Livurugwe - Geita

Balozi wa zao la pamba nchini Aggrey Mwanri, ameamrisha shamba la Jeremia Kisumo na Laher Robert wakazi wa Mshinde, Kata ya Bung’wangoko, mkoani Geita livurugwe na waanze kupanda upya zao hilo, baada ya kupanda bila kufuata mistari kama ambavyo serikali imewaelekeza.

 

Balozi Mwanri ametoa maamuzi hayo baada ya kufika kwenye shamba la mkulima huyo na kukuta amepanda mbegu za pamba bila mpangilio, licha ya wakulima hao kupewa elimu ya upandaji mbegu miezi mitatu iliyopita.

 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Renatus Luneja, amesema aina hiyo ya upandji haikubaliki na inasababisha hasara kwa mkulima huku akiwataka wakulima kupanda kwa kutumia mbegu chache na kufuata vipimo vya 30 kwa 60.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii