Mrembo Afungwa Jela Miezi 6 kwa Kutoboa Kondomu za Mpenzi Wake.

Mahakama moja nchini Ujerumani imemhukumu mwanamke mwenye umri wa miaka 39, kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu kondomu za mpenzi wake kimakusudi.
Katika uamuzi ambao hakimu aliutaja kuwa wa "kihistoria," mshtakiwa alidaiwa kutoboa mashimo kwenye kondomu za mpenzi wake bila yeye kujua.
Sababu ya kitendo hicho cha uhalifu kinachojulikana kama "stealthing"(kutoa kondomu bila idhini ya mwenzako wakati wa ngono) ni kuwa mwanamke huyo alitaka kupata mimba kinyume na ridhaa ya mwanamume.
Deutsewelle inaripoti kuwa mwanamke huyo alikuwa katika mpango wa "marafiki wenye manufaa" na mwanamume mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikutana naye mtandaoni mwaka wa 2021.
Kile ambacho kilikusudiwa kuwa uhusiano wa kawaida hata hivyo, kiligeuka alipoanza kuwa na hisia ya kimapenzi kwa mwanamume huyo.
Katika hatua iliyolenga kumnasa, mwanamke huyo alitoboa kwa siri mashimo kwenye kifurushi cha kondomu ambacho mwanamume huyo alikuwa nacho kwenye chumba chake.
Lakini mpango wake haukufaulu kwa sababu hakupata ujauzito na alikuwa amemjulisha mwanamume huyo kupitia WhatsApp kwamba alikuwa ameharibu kondomu zake kimakusudi.
Baada ya kukiri kwake, mwanamume huyo alimfungulia mashtaka ambapo aliungama kwamba alijaribu kumhadaa mpenzi wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii