Mwanamume Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 3 Jela kwa Kuiba Sahani 3.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 23, amehukumiwa kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kukiri mashtaka ya kuiba chupachai na sahani tatu za mama yake.
Kevin Okasimba, alikiri mashtaka hayo alipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mombasa Vincent Adet.
Katika kujitetea kwake, Okasimba aliambia mahakama kuwa aliiba vyombo hivyo kwa sababu alikuwa na njaa na alihitaji chakula ambacho mama yake hakuweza kumpatia.
Mahakama ilifahamishwa kuwa mnamo Mei 5, mwaka huu katika maeneo ya Changamwe, mlalamishi, Magreat Adudu alimuuliza mwanawe ikiwa ndiye aliyeiba vyombo vyake.
Ajaribu kumpiga mamake
Adudu alisema mwanawe alikereka na badala yake akatoka nje haraka na kurudi na panga na rungu na kutaka kumpiga.
Hakimu alimuuliza mshtakiwa sababu zake za kushindwa kujilisha na kujitegemea.
Kijana huyo alihukumiwa kutumikia kifungo cha miezi mitatu gerezani bila chaguo la faini na pia kupewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu yake.
Jamaa amuombea mama yake afe

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii