Kijana ambaye hajafahamika haraka
jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30 mkazi wa
Igoma halmashauri ya mji wa Njombe amenusurika kifo kutoka kwa wananchi
wenye hasira kali katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage mara baada ya
kukamatwa akiwa ameiba vitu mbali mbali Ikiwemo TV,Godoro,Blanketi na
Mtungi mdogo wa gesi.
Luo Lameck Mgeni ni mzee aliyekuwa
amempangisha awali katika nyumba yake kabla ya kumfukuza kutokana na
tabia ya wizi anasema anashangaa kuona kijana huyo ameondoka kwake
lakini amerudi na kuiba kwenye moja ya nyumba ya familia yake.
“Leo
nikasikia kule nyumbani wameboboa nikauliza wameiba nini,kuingia mle
ndani tukaona tandiko halipo na vitu vingine amechana chana ameweka
nje”alisema Mzee Mgeni
Hata hivyo kabla kijana huyo hajafikiwa
na hali mbaya kutokana na kipigo,Polisi imefika na kufanikiwa
kumuondosha katika eneo hilo.