Umoja wa Mataifa umesema waasi wa Houthi wameamua kutowatumia tena watoto kama wanajeshi. Waasi hao wamewatumia maelfu ya watoto kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa kwa miaka saba. Umoja wa Mataifa umesema waasi hao wametia saini kile kilichoelezewa kama
"mpango" wa kufikisha mwisho na kuzuia usajili na kutumiwa kwa watoto katika mapigano, kuwauwa ama kuwajeruhi na kushambuliwa shule na hospitali. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema waasi hao wamedhamiria kuwatambua watoto miongoni mwao na kuwaachia huru ndani ya miezi sita ijayo. Mmoja wa wanadiplomasia wakuu wa Wahouthi Abdul Eluh Hajaar ndiye aliyetia saini makubaliano hayo.