Israel yaidungua roketi iliyotokea Gaza

Jeshi la Israel linasema limedungua roketi iliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza jana. Hili ndilo shambulizi la kwanza la aina hiyo kufanyika baada ya miezi kadhaa wakati ambapo mivutano inazidi kuongezeka kati ya Waislamu na Wayahudi mjini Jerusalem. hakuna kundi lolote la Gaza lililodai kuhusika na shambulizi hilo lililofanyika kufuatia tahadhari kadha zilizotolewa na kundi la Kiislamu la Hamas kuhusiana na vitendo vya jeshi la Israel katika eneo la msikiti wa Al Aqsa. Duru kutoka Palestina zinasema masaa kadhaa baadae, jeshi la Israel lilifanya mashambulizi katika kambi zinazotumiwa na Hamas na kundi lengine lililoko huko Gaza. Jeshi hilo limesema lengo lao moja lilikuwa kiwanda kimoja cha kutengeneza silaha. Hakuna aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii