Watu wanane wakiwemo wanajeshi watatu wameuawa katika mji wa Bambu, Kilomita 40 kutoka mji wa Bunia, mkoani Ituri baada ya kupigwa risasi na mwanajesha aliyekuwa amelewa.
Kisa hiki kinazua wasiwasi miongoni mwa wanaharakati Mashariki mwa nchi hiyo, hasa katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri ambayo yapo chini ya uongozi wa kijeshi.
Kiongozi wa shirika la kiraia mkoani Ituri ; Dieudonné Losa, amesema mwanajeshi huyo alimpiga risasi wenzake kabla ya kuwageukia walinzi wawili na kuwauwa, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hali hii inazua wasiwasi kuhusu nidhamu ya wanajeshi wa DRC ambao wanapaswa kuwa katika mstari wa mbele kuwalinda raia, na msemaji wa Jeshi mkoani Itusr Luteni Jules Ngongo, amelaani koitendo hicho na kusema mwanajeshi huyo alikosa nidhamu.
Mwezi Julai mwaka 2020 , mwanajeshi mwengine aliyekuwa
amelewa, aliwauwa raia 14 mjini Sange huko Kivu Kusini na baadaye
akafungwa jema maisha.