MWANAMKE ANYWA MKOJO BADALA YA BIA

Huku wengine wakisumbuliwa na uraibu wa pombe na dawa za kulevya, basi kuna wengine ambao wana uraibu wa kunywa mkojo wao. Daah! ama kweli kila soko na wazimu wake.
 mwanamke mwenye umri wa miaka 53, ameleza kuwa ana uraibu wa kunywa mkojo wake mwenyewe.
Kulingana na mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Carrie, yeye hunywa mkojo wake kana kwamba yuko kwenye shindano la unywaji wa pombe na ni rahisi kwake kunywa mkojo kuliko maji.
Jinsi alianza kunywa mkojo wake
Carrie alibaini kuwa alianza kunywa mkojo wake na glasi moja tu asubuhi lakini sasa yeye hutumia hadi glasi tano kila siku.
Mama huyo amekuwa akinywa mkojo wake karibia miaka minne sasa.
Carrie alisema pia hutumia mkojo wake kupiga mswaki kwa sababu huifanya meno yake yawe meupe kutoka ndani.
Alipoulizwa iwapo mkojo wake hunuka, Carrie alijibu kuwa harufu hutegemea na kile alichokula.
"Inategemea nakile ninachokula, mkojo wangu unanuka. Ina ladha tofauti kabisa leo kuliko ilivyokuwa miaka minne iliyopita. Ina chumvi nyakati fulani, na champeni ya plum nyakati nyingine," alikiri.
Iliripotiwa kuwa, miaka minane iliyopita, mama huyo wa wasichana wanne aligunduliwa na kuwa na ugonjwa wa melanoma na hivyo alianza kunywa mkojo wake akiwa na matumaini ya kuharakisha kupona kwake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii