Mwanaharakati ahukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumtusi mfalme Mohammed

Mahakama moja ya Morocco Jumatatu imemuhukumu kifungo cha miaka minne jela mwanaharati aliyemtusi Mfalme Mohammed wa sita kwenye mitandao ya kijamii, wakili wake amesema.

“Rabie Al Ablaq amehukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kumkashifu mfalme mtandaoni,” wakili Abdelmajid Azaryah ameiambia AFP.

Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 11 Aprili baada ya Ablaq kuchapisha mtandaoni “ kanda za video zinazokosoa ukosefu wa usawa kati ya jamii na ufisadi,” wakili huyo amesema.

“Nimeshangazwa na hukumu hiyo kwa sababu alitoa maoni yake tu. Sikuhisi kwamba alihujumu taasisi ya kifalme,” ameongeza.

Wakili Azaryah amesema mwanaharakati huyo na mwanahabari wa masuala ya kijamii, mwenye umri wa miaka 35, aliombwa kulipa faini ya dirham 20,000, sawa na dola 2,000.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii