Waislamu kusherehekea Eid Mei 2 au 3

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limesema waumini wa dini na wananchi watashehekea sikukuu ya Eid el-Fitri Mei 2 au Mei 3 kulingana na mwandamo wa mwezi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Jumatatu Aprili 25, 2022, Katibu Mkuu wa Bakwata, Nuhu Mruma amesema sherehe za Eid el-Fitri kitaifa zitafanyika mkoa wa Dar es Salaam.

Mruma amesema swala la Eid itafanyika katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata makao makuu Kinondoni saa moja na nusu asubuhi.

“Baraza la Eid lifanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa nane mchana, kwa niaba ya Bakwata na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir tunawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” amesema Mruma.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii