Zaidi ya watu 100 wamekufa katika mlipuko wa kiwanda cha mafuta Nigeria

Zaidi ya watu 110 wameuawa kufuatia mlipuko uliotokea katika kiwanda haramu cha kuchakata mafuta kusini mashariki mwa Nigeria. Shughuli ya kutafuta miili inaendelea katika eneo hilo pamoja na kuwasaka watu wawili wanaoshukiwa kuhusika na mlipuko huo. Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema katika taarifa kuwa mlipuko huo ni msiba mkubwa na janga la kitaifa. Mlipuko huo wa Ijumaa usiku katika kiwancha cha eneo la Ohaji-Egbema jimbo la Imo ulisababishwa na moto katika maeneo mawili ya kuhifadhi mafuta ambako zaidi ya watu 100 waliokuwa wanafanya kazi. Rais Buhari ameviamuru vikosi vya usalama nchini humo kuimarisha msako wao dhidi ya viwanda vya aina hiyo vinavyofanya kazi kinyume cha sheria katika maeneo mengi ya kusini mwa Bigeria. Usafishaji haramu wa mafuta ni jambo la kawaida katika ukanda huo wa mafuta ambako wezi huharibu mabomba ili kuiba mapipa 200,000 ya mafuta ghafi kila mwaka ambayo wanayasafisha ili kuyauza kwenye soko la magendo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii