Mpatanishi mwandamizi kwa upande wa Ukraine na mshauri wa rais, Mykhailo Podolyak leo hii amesema majeshi ya Urusi bado yanaendelea kuushambulia mji wa Mariupol na kuhimiza Urusi kutekeleza makubaliano ya kuweka chini mtutu wa bunduki katika kipindi cha Pasaka ya madhehebu ya Orthodox.Kupitia ukurasa wake wa Twitter Podolyak amesema Urusi inaendelea kuishambulia Mariupol Azovstal. Eneo ambalo linajumuisha makazi ya raia na jeshi. Wanashambulia kwa makombora mazito ya anga na mizinga.Mshauri huyo wa rais pamoja na kuhimiza utii wa makubaliano ya kusitisha mapigano katika kipindi cha Pasaka, ametaka pia Urusi ifungue njia salama ya manusura na duru maalumu ya mazungumzo.