Mapigano yauwa watu wanane huko Darful

Mapigano kati ya kabila la waarabu na wakulima wa kabila la wachache katika eneo lililokumbwa na vita la Darfur nchini Sudan yamesababisha vifo vya watu wanane na wengine 16 kujeruhiwa. Mapigano hayo yalitokea siku ya Ijumaa katika eneo la Krink, takriban kilometa 80 kutoka mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi wa Geneina, wakati watu wa kabila la Waarabu waliokuwa na silaha waliposhambulia vijiji vya kabila la wachache wasiokuwa Waarabu la Massalit, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mauaji ya watu wawili wa kabila la waarabu. Msemaji wa shirika la kushughulikia wakimbizi huko Darful Adam Regal amesema, makumi ya nyumba zilichomwa moto huku idadi kubwa ya familia zikihamishwa. Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, mzozo huo uliozuka mwaka wa 2003 kati ya waasi wa kabila dogo na serikali inayoongozwa na Waarabu mjini Khartoum na uliua watu 300,000 na wengine milioni 2.5 kuwa wakimbizi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii