Kalenda ya Saudi Arabia ya mwaka 2030 inaonesha kwamba Waislamu katika mwaka huo watafunga mara mbili kwa mwaka
kwa
mujibu wa mtaalamu wa Nyota Khalid al-Zaqaq, tofauti ya siku za hesabu
hizo ina maana kwamba kila baada ya miaka thelathini mfungo wa
ramadhani hutokea mara mbili kwa mwaka.
Unapotazama kalenda ya
Saudi Arabia 2030 unaona kwamba Ramadhani ya kwanza itaanza Januari 6,
huku Eid ikiangukia tarehe 5 Februari. Ramadhani ya pili inaangukia
tarehe 26 Disemba mwaka huo huo.