Mamia wapoteza maisha katika mafuriko nchini Afrika Kusini

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko kwenye maeneo ya mji wa Durban nchini Afrika Kusini imepanda na kufikia 259. Mamlaka nchini humo zinasema watu wengi zaidi bado wanahofiwa kupotea. Mvua zilizonyesha kwa siku kadhaa zimesababisha maporomoko ya udongo na kusomba makaazi ya watu. Idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka wakati zoezi la utafutaji na uokoaji likiendelea katika jimbo la KwaZulu-Natal. Raia wengi wa maeneo hayo wamelazimika kuyakimbia makaazi yao ambayo yamesombwa na maji, majengo kuporomoka na miundombinu ya barabara kuharibika vibaya. Bandari ya Durban ilifurika maji na kontena za meli kusombwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii