Maunda Zorro Afariki Dunia kwa Ajali ya Gari Usiku wa Kuamkia Leo Dar

MSANII wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari, usiku wa kuamkia leo, April 14, 2022 baada ya gari alilokuwa amepanda aina ya VITZ kugongana uso kwa uso na lori la mchanga Kigamboni, Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu ambaye pia ni msanii wa Bongofleva, Banana Zorro, akizungumza na chombo kimoja cha habari, amethibitisha taarifa hizo na kusema hadi jana jioni alikuwa pamoja na Maunda kwenye msiba wa rafiki yao lakini baadaye akapata taarifa kuwa Maunda amefariki.

Msanii wa Bongo Flava, Banana Zoro ametoa taarifa ya kinachondelea kuhusu msiba wa Maunda Zorro kwa kueleza kwamba kwa sasa msiba upo Maweni Kigamboni kwa Mzee Zorro na taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.

Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa taarifa zaidi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii