AMUUA MTOTO WA MDOGO WAKE.

Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi hilo linamshikilia Latifa Bakari (33) mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne baada ya kumpiga kupita kiasi.

kamanda muliro amesematukio hilo limetokea tarehe tano na baada ya mtuhumiwa kutekeleza kitendo hicho akauweka mwili wa mtoto huyo katika ndoo kwa lengo la kuuficha .

Pia kamanda murilo ameongeza kuwa kufuatia taarifa njema za majirani ndizo zilizofanikisha kumnasa mtuhumiwa na upelelezi utakapokamilika  atafikishwa mahakamani .

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii