Urusi na Ukraine zimeshambuliana siku ya Alhamisi Alfajiri, siku moja tu baada ya mazungumzo ya amani kati ya maafisa wa nchi zao kukukutana na wajumbe wa Marekani.
Milipuko imesikika katika jiji la Kyiv nchini Ukraine, huku waliosikia wakisema hawawezi kueleza ni kwa kiasi gani kumekuwa na uharibifu.
Urusi nayo imeangusha ndege tano zisizokuwa na rubani, zilizorushwa jijini Moscow, kwa mujibu wa Meya wa jiji hilo Sergei Sobyanin, lakini hakutoa maelezo ya kina.
Baada ya mazungumzo ya Jumatano jijini Abu Dhabi katika nchi ya Falme za Kiarabu chini ya wajumbe wa Marekani Jared Kushner na Steve Witkoff, pande zote zilikubaliana kubadilishana wafungwa katika wiki zijazo.
Wajumbe hao wa Marekani sasa wanatarajiwa kwenda jijini Moscow kukutana na rais Vladimir Putin kumshawishi kukubali wawakilishi kutoka barani Ulaya, kushiriki kwenye mazungumzo hayo, kabla ya kukutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy jijini Dublin nchini Ireland.
Zelenskyy amesisitiza kuwa Ulaya lazima iwe kwenye meza ya mazungumzo ili kupata mkataba wa kuaminika wa amani.