Mpango wa kumuondoa madarakani Waziri wa ulinzi umefeli

Nchini Marekani mpango wa  kumwondoa madarakani Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth, kupitia kura ya kukosa imani naye umegonga mwamba baada ya idadi kubwa ya wabunge katika Baraza la wawakilishi kupiga kura ya kutaka suala hilo kupelekwa kwenye kamati ya bunge.

Mswada huo ulishindwa baada ya wabunge wengi wa Republican 211 ambao kwa sasa ni wengi hadi mwezi Januari, kupinga mpango huo, huku 204 kutoka chama cha Democratic wakiunga mkono.

Wabunge kutoka Democratic walitaka Pete Hegseth, kuondolewa madarakani wakimtuhumu kwa vita vya Iran, ambapo jeshi la Marekani lilishiriki bila idhini ya Congress pamoja na mambo mengine.

Hatua hii inamaanisha kuwa, kwa sasa mswada dhidi ya Waziri huyo, hauwezi kuendelea, kuelekea mwezi Januari mwaka ujao, wakati chama cha Democratic kitadhibiti bunge hilo.

Hegseth amesema mpango huo wa kujaribu kumwondoa madarakani ni kitendo cha kuigiza na mpango wa makusudi wa wapinzani wa serikali ya Marekani.

Rais Donald Trump, amefurahishwa na uamuzi huo akisema, jitihada za wapinzani zimegongwa mwamba kwa aibu kubwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii