DCEA yakamata paketi 299 za dawa za kulevya Mwenge

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata paketi 299 za dawa za kulevya, zikiwemo paketi 24 za heroin na 275 za methamphetamine, katika operesheni iliyofanyika Novemba 6, 2026, eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam.

Dawa hizo zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya magari mawili aina ya Ford Ranger yenye namba za usajili T.950 ERA na T.417 EJZ. Magari hayo pia yamekamatwa na kushikiliwa kwa tuhuma za kuhusishwa na usafirishaji wa dawa hizo.

Katika operesheni hiyo, watu wanne walikamatwa. Watuhumiwa hao ni Juma Slaati Kisomeko (36), raia wa Uganda, dereva na mkazi wa Piji nchini humo; Issa Said Nassoro (34), mfanyabiashara; Ibrahim Said Chembela (30), dereva; na Mohamed Ally Shemtuu (45), dereva.

Watuhumiwa watatu wa mwisho ni wakazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii