Raia wa Afrika Kusini wanashiriki uchaguzi wa mitaa

Raia wa Afrika Kusini, hivi leo wanapiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, uchaguzi ambao unatarajiwa ama kukiimarisha chama tawala ANC au kukidhoofisha kabisa kuelekea uchaguzi mkuu ujao wa Urais na wabunge.

Katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2021, umaarufu wa chama tawala ANC ulipungua kwa asilimia 50, kura za maoni zikionyesha kwamba huenda mwaka huu ukapungua hadi asilimia 40.

Raia wa Afrika Kusini wamekuwa wakiituhumu serikali kwa kushindwa kutatua changamoto zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji na kukatika mara kwa mara kwa umeme.

Aidha inahofiwa kwamba huenda kusiwe na chama ambacho kitapata idadi kubwa ya wawakilishi kwenye uchaguzi wa leo ambapo vyama mbalimbali vitalazimika kuungana ili kuwa na idadi inayohitajika katika bunge.

Matokeo ya uchaguzi wa leo yanatarajiwa kuwa kipimo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2029.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii