Raia wa Uganda, wanaorejea nyumbani kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watalazimika kukaa karatini kwa siku 21, katika jitihada za kupambana na maambukizi ya Ebola.
Wizara ya afya imetangaza hatua mpya kulenga wanainchi wa Kongo ikiwemo kupiga marufuku safari za moja kwa moja au kupita nchini Uganda, hata kwa kutumia ndege zilizokodiwa kuwakamata wale wanaoingia kinyume cha sheria, kuwafukuza nchini kwa gharama zao, na kuwapa adhabu kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Uganda zimetangazwa na waziri wa faya Dk Chris Baryomunsi
“Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaoingia Uganda kwa safari zisizo za muhimu watarudishwa DRC kwa gharama zao wenyewe na wasafiri wenye historia ya kusafiri kwenda DRC hawataruhusiwa kupita nchini Uganda kwa kutumia njia yoyote ya usafiri, ikiwemo ndege zilizokodiwa” Amesema Chris Baryomunsi, Waziri wa Afya wa Uganda.