Wanajeshi wa mwisho wa Marekani wanaondoka Iraq

Baada ya kuwasili nchini Iraq mwaka wa 2003 kumpindua rais wa nchi hiyo Saddam Hussein na baadaye kuwa kikosi kinachoongoza katika muungano wa kimataifa unaopigana na kundi la Islamic State, jeshi la Marekani litaondoka kutoka kwenye kambi zake za mwisho zilizobaki nchini Iraq leo Jumatano, Septemba 30. Kujiondoa huku, kulioamuliwa na Joe Biden mwaka wa 2024, kunakuja katika muktadha wa vita kati ya Israel na Marekani vilivyoanzishwa mwezi Februari mwaka huu dhidi ya Iran.

Iraq inafunga ukurasa wa miaka 20 ya uwepo wa jeshi la Marekani nchini humo. Siku ya Jumatano, Septemba 30, 2026, jeshi la Marekani linajiondoa kutoka kwenye kambi zake za mwisho nchini Iraq.

Marekani iliingia Iraq mnamo 2003 ili kumuondoa Saddam Hussein.  Wanajeshi 4,500 wa Marekani walipoteza maisha tangu kuwasili kwao nchini humo.  Baadaye, Marekani iliongoza muungano wa kimataifa kupambana na kundi la Islamic State (ISIS), ambalo liliibuka wakati wa machafuko hayo.  Hatua hii inahitimisha rasmi uwepo wa kijeshi wa Marekani uliodumu kwa miongo miwili, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ushawishi wa nchi jirani ya Iran na usalama wa baadaye nchini Iraq.

Iliamuliwa mwaka wa 2024 na Rais Joe Biden, kuondoka kwa jeshi la Marekani nchini Iraq ni matokeo ya makubaliano yaliyosainiwa na Baghdad na Washington ambayo pia yalibainisha kupokonywa silaha kwa makundi yenye silaha yanyoyounga mkono Iran, ambayo Waziri Mkuu mpya wa Iraq aliahidi kwamba yatapokonywa silaha ifikapo Juni 2027, katika jaribio la kumridhisha mshirika wa Marekani.

Kwa Iraq, ambayo imekuwa ikijaribu kwa miaka mingi kujikomboa kutokana na kuingiliwa na wafadhili wake wawili wakuu na ambayo eneo lake limekuwa uwanja wa mapigano katika uhasama wao, kuondoka kwa wanajeshi wa mwisho wa Marekani kunakuja katika muktadha wa kutokuwa na utulivu. Ukosefu huu wa utulivu ni mkubwa zaidi kwa sababu—tangu Donald Trump alipoona inafaa kuiwasilisha kama njia inayowezekana ya kuzindua mashambulizi ya ardhini dhidi ya Iran—Kurdistan ya Iraq, pamoja na vituo vya muungano wa kimataifa, vinalengwa mara kwa mara na Tehran na washirika wake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii